Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, desturi njema ya mkopo usio na riba ni miongoni mwa maelekezo makuu ya kiuchumi katika Uislamu, kwa lengo la kutatua matatizo ya maisha na kuimarisha mahusiano ya kifamilia. Hata hivyo, ufahamu sahihi wa mipaka yake ya kifiqhi ni wa lazima ili kujiepusha na shaka ya riba na kulinda usafi wa mali. Katika taarifa hii, jibu la kifiqhi la Hujjatul-Islam wal-Muslimin Aliyan-Nejad, kwa kuzingatia fatwa ya Ayatullah Makarem Shirazi, limefafanuliwa.
Swali
Nimemkopesha mkwe wangu tomani milioni [50], naye anasema atanirudishia tomani milioni [5] zaidi ya kiasi cha awali, kama shukrani kwa kitendo hicho. Je, jambo hili linaruhusiwa kifiqhi na halihesabiwi kuwa riba?
Jibu
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Aliyan-Nejad, akieleza fatwa ya Ayatullah Makarem Shirazi kuhusu suala hili, amejibu:
Iwapo jambo hili liliwekwa kuwa sharti tangu mwanzo, basi ni riba na ni haramu. Katika aya nyingi za Qur’ani Tukufu na riwaya nyingi za Maasumu (a.s.), kitendo hiki kimekemewa vikali, na huondoa baraka katika maisha.
Lakini iwapo jambo hilo kama halikuwekwa sharti wakati wa kutoa mkopo, na mkopaji kwa hiari yake anataka kumlipa mkopeshaji kiasi cha ziada kwa namna ya shukrani na kuthamini, basi si tu kwamba hakuna tatizo wala katazo katika hilo, bali pia limehimizwa na linahesabiwa kuwa ni tendo linalopendekezwa.
Maelezo ya masuala yanayohusu riba yanaweza kusomwa katika kitabu Riba na Benki cha Ayatullah al-Udhma Makarem Shirazi (Mwenyezi Mungu aendeleze kivuli chake).
Maoni yako